Faharasa

Kiswahili

achano
Mraba ya mbali ya kawaida kutoka wastani. Kuipata, tengua nambari na wastani ya nambari hizo, halafu kokotoa wastani ya mraba.
Deutsch, English, Español, Italiano
amri
Agizo la kuiambia programu ya kompyuta kufanya kazi maalum.
English, አማርኛ
ASCII
Njia ya kawaida ya kuwakilisha herufi zinazotumiwa sana katika lugha za Ulaya Magharibi kama nambari kamili 7- au 8-bit, ambayo sasa imechukuliwa na Unicode.
Afrikaans, Deutsch, English, Español, Français, አማርኛ, اَلْعَرَبِيَّةُ

B

biti
Sehemu ya habari inayowakilisha njia mbadala, ndiyo/hapana, true/false. Katika kuhesabu hali ya 0 au 1.
binary, Boolean
Afrikaans, Deutsch, English, Español, Français, Português, Nederlands, Setswana, አማርኛ, Bahasa Indonesia
boilerplate
Maandishi ya kawaida ambayo yanajumuishwa katika mikataba ya kisheria, leseni, na kadhalika. Pia sehemu za msimbo wa chanzo ambazo zinapaswa kurudiwa mara nyingi sana ili kupata utendakazi msingi. Katika object-oriented programs sehemu hizi hutumika kujumuisha viambajengo vya vitu. Lugha zingine zinahitaji mengi ya kauli hizi na huitwa lugha za boilerplate, k.m. Java, ambayo ina maana kwamba huzalishwa kiotomatiki mara kwa mara au kwa kutumia auto-completion.
Deutsch, English, አማርኛ
Boolean
Kuhusiana na aina au aina ya data ambayo inaweza kuwa na thamani ya kimantiki ya true au false. Imetajwa kwa George Boole, mwanahisabati wa karne ya 19. Mifumo ya binary, kama kompyuta zote, imejengwa juu ya msingi huu wa mifumo ya tathmini ya kimantiki kati ya majimbo ya kweli na ya uwongo, 1 au 0.
truthy, uongo, binary
Deutsch, English, Español, Português, አማርኛ, اَلْعَرَبِيَّةُ, Bahasa Indonesia

C

Central Processing Unit
Vifaa vikuu vya kompyuta yoyote ya dijitali inayojumuisha sakiti muhimu za kielektroniki zinazotafsiri na kutekeleza maagizo kutoka kwa programu au maunzi mengine.
gpu
Deutsch, English, አማርኛ

D

Data Fremu
Muundo wa data wa pande mbili wa kuhifadhi data ya tabular katika kumbukumbu. Safu zinawakilisha rekodi na nguzo zinawakilisha vigezo.
tidy_data
English, Español, Français
Data kubwa
Data inahitaji kutumikwa kwa kichakato kizito.
three_vs
Afrikaans, Deutsch, English, Setswana, አማርኛ, اَلْعَرَبِيَّةُ

F

faili ya usanidi
Faili inayobainisha vigezo na mipangilio ya awali ya programu. Faili ya usanidi hutumiwa kwa habari zinazobadilika mara nyingi, kama vile mipangilio iambatanayo ya mazingira.
English, አማርኛ
FASTA
Umbizo la faili la kuhifadhi amino asidi au taarifa ya mfuatano wa jeni. Habari kwa kila mlolongo imegawanywa katika kizuizi cha mistari miwili(2). Mstari wa kwanza (1) una taarifa kuhusu mfuatano na huanza na alama kubwa kuliko, ‘>’. Mstari wa pili (2) una asidi ya amino halisi au mfuatano wa jeni kwa kutumia misimbo ya herufi moja.
English
FASTQ
Umbizo la faili la kuhifadhi maelezo ya mfuatano wa jeni na alama za ubora zinazolingana. Habari kwa kila mlolongo imegawanywa katika kizuizi cha mistari minne. Mstari wa kwanza (1) una taarifa kuhusu mfuatano huo na huanza na ‘@’. Mstari wa pili (2) una mfuatano halisi wa jeni kwa kutumia misimbo ya herufi moja kuwakilisha nyukleotidi. Mstari wa tatu (3) ni kitenganishi kinachoanza na +. Mstari wa nne (4) una mfuatano wa herufi za ubora kwa kila msingi katika mfuatano wa jeni.
English

H

Hali ya Kuambatanisha
Kuongeza data mwishoni mwa faili iliyopo badala ya kubatilisha yaliyomo awali ya faili hiyo. Kuandika upya ni chaguo-msingi, kwa hivyo lugha nyingi za programu ahitaji programu kuwa wazi kuhusu kutaka kuambatanisha badala yake.
Afrikaans, English, አማርኛ
hali
Hitilafu au tukio lingine lisilotarajiwa ambalo linatatiza mtiririko wa kawaida wa udhibiti.
handle_condition
Afrikaans, English, አማርኛ
hifadhidata ya uhusiano
Hifadhidata ambayo hupanga habari katika majedwali, ambayo kila moja ina seti isiyobadilika ya sehemu zilizotajwa (zinazoonyeshwa kama safu wima) na idadi tofauti ya rekodi (zinazoonyeshwa kama safu mlalo).
sql
English, Español, Français
Hoja
Neno hilo halipaswi kuchanganywa na, na si kisawe cha,parameter. Hoja ni mojawapo ya misemo kadhaa ambayo hupitishwa kwa chaguo la kukokotoa. Ni thamani halisi inayopitishwa. Vigezo na hoja ni tofauti, lakini dhana zinazohusiana. Vigezo ni vigeuzo na hoja ni thamani zilizopewa vigeu hivyo.
Afrikaans, Deutsch, English, Español, Français, Português, አማርኛ, اَلْعَرَبِيَّةُ

I

isimu ya hesabu
Utafiti au utumiaji wa mbinu za kukokotoa na kuchanganua au kuelewa lugha za binadamu. Mbinu za awali zilikuwa za algorithmic; mbinu nyingi za kisasa ni za takwimu.
nlp
English, Español, አማርኛ
isiyolingana
Haifanyiki kwa wakati mmoja. Katika programu, operesheni ya asynchronous ni ile inayoendesha kwa kujitegemea ya nyingine, au ambayo huanza wakati mmoja na kuishia kwa mwingine.
synchronous
Afrikaans, Deutsch, English, Español, Français, አማርኛ, اَلْعَرَبِيَّةُ

K

Kabrasha
Neno lingine kwa saraka.
Deutsch, English, Español, አማርኛ
Kifurushi cha data
Kifurushi cha programu ambacho, mara nyingi, kina data pekee. Hutumika kurahisisha kusambaza data kwa matumizi rahisi.
Afrikaans, English, አማርኛ
Kigezo
Tabia au ubinafsi wa kitu ambacho kinaweza kupimika (kama vile urefu, kimo, idadi ya petali) na kutumika kama ingizo la modeli. Kutafuta au kuchagua vipengele ambavyo ni huru na vibaguzi ni sehemu ya msingi ya uainishaji.
English
kingo
Muunganisho kati ya [nodes] mbili (#node) katika graph. Kingo yanaweza kuwa data inayohusishwa nayo, kama vile jina au umbali.
English, አማርኛ
Kiolesura cha Kuandaa Programu [API]
Seti ya vipengele na taratibu zinazotolewa na maktaba moja ya programu au huduma ya tovuti ambayo programu nyingine inaweza kuwasiliana nayo. API sio msimbo, hifadhidata, au seva: ni mahali pa ufikiaji.
Afrikaans, Deutsch, English, Español, Français, Setswana, አማርኛ, اَلْعَرَبِيَّةُ
kipengele (katika programu)
Baadhi ya vipengele vya programu ambavyo viliundwa au kujengwa kimakusudi. [hitilafu] (#bug) ni kipengele kisichohitajika.
English, አማርኛ
kishawishi endelevu
kishawishi kinachoashiria kwamba amri inayochapwa kwa sasa bado haijakamilika, na itaendeshwa mara tu itakapokamilika.
English, አማርኛ
kitu kikubwa cha binary
Data ambayo imehifadhiwa katika hifadhidata bila kufasiriwa kwa njia yoyote, kama vile faili ya sauti. Neno hili pia sasa linatumika kurejelea data iliyohamishwa kupitia mtandao au kuhifadhiwa katika version control repository kama biti zisizotafsiriwa.
English, Setswana
koni ya kompyuta
Kituo cha kompyuta ambapo mtumiaji anaweza kuingiza amri, au programu, kama vile shell ambayo huiga kifaa kama hicho.
English, አማርኛ
kuasisi msimbo (majaribuni)
Ni kiasi gani maktaba au programu imetekelezwa wakati wa majaribio. kwa mfano, ikiwa mistari 40 kati ya 50 ndani faili imetekelezwa wakati wa majaribio, majaribio hayo yana kiwango cha asilimia 80%.
English, አማርኛ
kugawanya
Mchakato wa kugawanya data katika vikundi wakati vikundi vyenyewe bado havijagunduliwa mapema.
centroid, classification, supervised_learning, unsupervised_learning
English, Português, አማርኛ, 日本語
kujifunza kwa kina
Familia ya algoriti za mtandao wa neva neural network ambazo hutumia tabaka nyingi ili kutoa vipengele katika viwango vya juu.
English, አማርኛ
kukamilika kiotomatiki
Kipengele kinachomruhusu mtumiaji kumaliza neno au msimbo haraka kwa kubofya kitufe cha TAB ili kuorodhesha maneno au msimbo unaowezekana ambao mtumiaji anaweza kuchagua.
Afrikaans, Deutsch, English, Español, Français, Português, አማርኛ
kupunguza
Operesheni isiyo ya kawaida ambayo hupunguza thamani ya kigezo, kwa kawaida kwa 1.
increment
English, Español, Português
kura ya chini
Kura dhidi ya kitu.
up_vote
English, አማርኛ
Kusababisha
Uhusiano kati ya matukio tofauti, ambapo inadaiwa kuwa tukio moja linawajibika kuzalisha au kuathiri mabadiliko katika nyingine.
Deutsch, English, Français, አማርኛ
kushindwa (jaribio)
Jaribio litashindikana ikiwa matokeo_halisi hayalingani na matokeo_yanayotarajiwa
pass_test
English, Español, Setswana, አማርኛ
Kutambulisha
Kuwa na marejeleo mawili au zaidi ya kitu kimoja, kama vile muundo wa data kwenye kumbukumbu au faili kwenye diski.
Afrikaans, Deutsch, English, Setswana

M

maarifa ya kikoa
Uelewa wa kikoa maalum, kwa mfano, ujuzi wa vifaa vya usafiri.
English, አማርኛ
Madai
Semi ya Boolean ambayo lazima iwe true katika hatua fulani katika programu. Madai yanaweza kujengwa katika lugha (k.m., kauli ya assert ya Python) au kutolewa kama vitendakazi (k.m., stopifnot ya R). Mara nyingi hutumiwa katika majaribio, lakini pia huwekwa katika production code ili kuangalia ikiwa inatenda ipasavyo. Katika lugha nyingi, madai hayafai kutumiwa kutekeleza uthibitishaji wa data kwa vile yanaweza kuondolewa kimyakimya na wakusanyaji na wakalimani chini ya hali ya uboreshaji. Kutumia madai kwa uthibitishaji wa data kwa hivyo kunaweza kuanzisha hatari za usalama. Tofauti na lugha nyingi, R haina taarifa ya assert ambayo inaweza kuzimwa, na kwa hivyo matumizi ya package kama vile assertr kwa uthibitishaji wa data haileti mashimo ya usalama.
Afrikaans, Deutsch, English, አማርኛ
maendeleo pesi
Mbinu ya ukuzaji programu ambayo inasisitiza hatua nyingi ndogo na maoni endelevu badala ya mipango ya mbeleni na ratiba ya muda mrefu. Exploratory programming mara nyingi huwa chapa.
Afrikaans, Deutsch, English, Español, Português, Setswana
Maoni Mapana
Maoni comment ambayo yanajumuisha mistari mingi. Maoni mapana yanaweza kuwekewa alama maalum za kuanza na kumalizia, kama vile /* na */ katika C na vizazi vyake, au kila mstari unaweza kuanikwa kwa alama kama #.
Deutsch, English, Português, አማርኛ
maoni
Maandishi yaliyoandikwa kwa hati ambayo hayachukuliwi kama kanuni ya kutekelezwa, lakini kama maandishi ambayo yanaelezea kile kanuni hufanya nini. Mara nyingi, hati hizi huwa na maelezo mafupi, yanayoanza na # (katika lugha nyingi za programu).
Deutsch, English, Français, Português, አማርኛ
maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Orodha iliyoratibiwa ya maswali yanayoulizwa kwa kawaida kuhusu mada fulani, pamoja na majibu.
English, አማርኛ
matokeo halisi
Huonyesha matokeo ya kujaribu msimbo kwenye tarakilishi. Ikiwa hili linafanana na [matokeo halisi] (#expected_result), hilo jaribio hupita; Ikiwa upatalo na matokeo halisi sio sawa, huo msimbo huwa jaribio lililoshindikana
Afrikaans, Deutsch, English, Español, Setswana, اَلْعَرَبِيَّةُ, Bahasa Indonesia
matokeo yanayotarajiwa (ya majaribio)
Thamani ambayo kipande cha programu kinatakiwa kutoa kinapojaribiwa kwa njia fulani, au hali ambayo kinatakiwa kuondoka kwenye mfumo.
matokeo halisi
English, Español, አማርኛ
mazingira
Muundo unaohifadhi seti ya majina tofauti na thamani wanazorejelea.
English, Français, አማርኛ
mchakato wa data
Jina la mazungumzo kwa kiwango kidogo cha data engineering.
English, አማርኛ
mchanganyiko
Kugawana vitu mingi pamoja, kwa mfano, kujumlisha nambari au kunganisha matini.
Afrikaans, English, Español, Français, Português, Setswana, اَلْعَرَبِيَّةُ
Mpangilio orodha
Kipengee ndani ya mfumo wa faili ambao unaweza kuwa na faili na saraka zingine. Pia inajulikana kama folda.
English, Español
muundo wa data
Muundo wa ushirikashi, usimamizi na ufikiaji bora wa data. Kwa kawaida itakuwa kubainisha thamani ya seti za data na uwakilishi wao (au encoding), uhusiano kati ya thamana, na njia za kufikia au kuendesha data hizo, kama vile kusoma, kubadilisha, au kuandika.
English
mwanasayansi wa data
mtu anayetumia ujuzi wa programu kutafuta suluhu/kusuluhisha matatizo ya takwimu.
Afrikaans, Ελληνικά, English, Español, Português, አማርኛ

O

Ombi la kuongeza Kigezo (au kipengele)
Ombi kwa watunzaji au wasanidi programu wa kuongeza utendaji maalum (au kipengele) kwenye programu hiyo.
English, አማርኛ

P

programu ya uchunguzi
Mbinu ya uundaji wa programu ambayo mahitaji huibuka au kubadilika jinsi programu inavyoandikwa, mara nyingi kwa kujibu matokeo ya uendeshaji wa mapema.
English, Español, አማርኛ

S

safu ya ushirika
Rejelea dictionary.
Afrikaans, Deutsch, English, አማርኛ
sayansi ya data
mchanganyiko wa takwimu, programu na kazi ngumu inayotumika kupata maarifa kutoka kwa data.
Afrikaans, Ελληνικά, English, Español, Português, አማርኛ
sifa
Jozi ya thamani ya jina inayohusishwa na kitu, inayotumiwa kuhifadhi metadata kuhusu kitu kama vile vipimo vya mkusanyiko.
Afrikaans, Deutsch, English, Español, Français, Setswana, አማርኛ, Bahasa Indonesia

T

taswira ya data
Uundaji wa chati, ramani, grafu, au infographics ili kutafsiri seti za data kuwa kitu kinachoonekana. Wakati mwingine huitwa “dataviz” au “data viz.”
English, አማርኛ
tathmini
Mchakato wa kuchukua usemi kama vile 1+2*3/4 na kuugeuza kuwa thamani moja isiyoweza kupunguzwa.
English, አማርኛ
tawi
rejelea Git branch.
English, አማርኛ
thabiti
Thamani ambayo haiwezi kubadilishwa baada ya kubainishwa, ukilinganisha na kigeu ambayo hubadilika.
English, Español, Français, اَلْعَرَبِيَّةُ

U

Uchimbaji data
Mchakato wa kuchimba na kugundua mifumo katika seti kubwa za data kwa kutumia tarakilishi.
Afrikaans, English, IsiZulu, አማርኛ
uhusiano wa kiotomatiki
Kiwango cha ufanano kati ya uchunguzi katika mfululizo sawa lakini ukitenganishwa na muda (unaojulikana kama lag). Uchanganuzi wa uunganisho otomatiki unaweza kutumika kupata maarifa kuhusu mkusanyiko wa data wa mfululizo wa saa kwa kugundua ruwaza zinazorudiwa ambazo zinaweza kufichwa kwa kiasi na kelele nasibu, miongoni mwa matumizi mengine.
English
ukubwa wa nambari ya ukosefu
Ukubwa wa hesabu ya kutoa jibu umepata kutoka jibu sahihi. Dhani ingine kama hii, ni uwiano wa ukosefu.
Afrikaans, Deutsch, English, Español, Français, Italiano, Português, አማርኛ, اَلْعَرَبِيَّةُ, Bahasa Indonesia
uongo hasi
Pointi za data ambazo kwa hakika ni za kweli lakini zimetabiriwa kimakosa kama kua za uongo.
uwongo chanya, true_negative, true_positive, machine_learning, classification
English
uongo
Mantiki ya Boolean iliyo katika hali kinyume cha kweli. Inatumika katika mantiki na upangaji kuwakilisha hali binary ya kitu.
truthy, uongo
English, አማርኛ
uongo
Inatathmini hadi ya uongo katika muktadha wa Boolean.
truthy
English, አማርኛ
usahihi
Kipimo cha takwimu cha muundo wa uainishaji ambao hutoa uwiano ya utabiri sahihi kati ya jumla ya idadi ya kesi. Imehesabiwa kama Usahihi = (TP+TN)/(TP+TN+FP+FN)
English, Español
utatuzi
Katika mazingira ya kompyuta ‘utatuzi’ inarejelea mchakato wa kutafuta na kutatua makosa (pia hujulikana kama hitilafu) ndani ya programu au mifumo ya kompyuta.
English
utegemezi
hali ya kutegemea jambo ama kitu fulani
English, አማርኛ
uwezesho
Sifa ya kitu ambacho kinapendekeza jinsi kinavyoweza kutumika, kama vile mpini au kitufe.
Afrikaans, English, አማርኛ, Bahasa Indonesia
uwongo chanya
Pointi za data ambazo kwa hakika ni za uongo lakini zimetabiriwa kimakosa kama kua za kweli.
uongo hasi, true_negative, true_positive, machine_learning, classification
English

W

wastani wa hesabu
Rejelea mean. Imehesabiwa kutoka kwa seti ya nambari za n kwa kujumlisha nambari hizo, na kugawanya matokeo na
Afrikaans, English, Español, Italiano, Português, አማርኛ
wastani
Namba ya katikati kwa data. Kuikokotoa, jumla nambari halafu gawana na nambari za nambari.
median, mode
Afrikaans, Deutsch, English, Italiano, Português, አማርኛ